JINA LA
BIASHARA_Faida zake na Namna ya Kusajili
Jina la Biashara, ukiwa wewe mwenyewe.
Je, wewe ni mfanyabiashara? Biashara yako yako ina
jina la Biashara. Kama jibu ni âHAPANAâ makala hii ni muhimu sana kwako!
Je, umewahi kusikia chochote kuhusu Usajili wa Jina
la Biashara?
Je, Jina la Biashara yako imesajiliwa? Kama jibu ni âHAPANAâ
makala hii ni muhimu sana kwako!
Je, ungetamani sana kulisajili Jina la Biashara,
lakini haujui namna gani ya kusajili?
Nasema ni muhimu kwa sababu, mara baada ya kuisoma makala
hii kwa umakini, utaelewa mambo mengi
sana ikiwemo faida za jina la biashara, Kwanini jina la biashara pamoja na
hatua za kulisajili jina lako la biashara.
Kabla ya kukupa majibu ya maswali yako, Soma kwanza
stori hii ya Ukweli kuhusu mimi.
Mwaka 2020, ndipo niliposikia kuhusu Usajili wa Jina
la Biashara kupitia BRELA ORS, kupitia mafunzo ya kundi la whatsApp. Nilielezwa
faida zake za kusajili jina la Biashara, sifa za jina linalokubalika kisheria
na vitu vinavyopaswa kuwa navyo ili kufanikisha hilo.
Mara baada ya kuelewa kuhusiana na Jina la Biashara,
nilianza kufuatilia usajili wa jina la Taasisi yangu inayoitwa âELIMU KITAA
FOUNDATIONâ. Niliweza kusajili jina hilo kupitia BRELA ORS kwa gharama kubwa
kidogo na hii ilichagizwa na kutofahamu kwamba naweza kufanya mwenyewe bila
kumlipa mtu.
Siku moja nilianza kufuatilia namna ambavyo usajili
huu kupitia BRELA unafanyika. Ndipo nilipoweza kusajili jina la biashara yenye
jina âJFG ENTERPRISESâ kwa gharama nafuu zaidi na kuweza kuokoa zaidi ya Tsh
30K.
Hii ndiyo sababu iliyonisukuma kuandika kitabu hiki ili
kukusaidia wewe kufanya usajili wa Jina la biashara, kampuni na alama za bidhaa
au huduma.
KITABU hiki ni suluhisho kwako na ni muhimu zaidi
kwako rafiki yangu. Kwa sababu itakupunguzia gharama ambazo ungepaswa kulipa kwa
wale ambao watakusaidia kufanya hilo. Pia utaweza kufanya usajili ukiwa wewe
mwenyewe ukiwa popote!
BONYEZA HAPA KUPATA MAELEZO ZAIDI
Je, JINA LA BIASHARA ni nini?
Jina la biashara ni utambulisho ambao umeamua
biashara yako ifahamike/biashara na kuitwa kwa jina hilo.
Jina la biashara ni jina ambalo hutumika
kutambulisha bidhaa, huduma au shughuli za biashara.
Jina la biashara ni utambulisho wa huduma, bidhaa au
shughuli zako.
Jina unalotumia katika biashara yako, Mfano MARIAM
BEAUTY SALON, JFG ENTERPRISES na kadhalika, linaitwa jina la Biashara.
Jina hilo si halali, kama halijasajiliwa, pia si
jina lako kwa kuwa yeyote anaweza kulitumia jina hilo, jambo ambalo linapelekea
mkanganyiko kwa wateja wako.
Unaweza pia kulipoteza jina hilo endapo mtu mwingine
akajitokeza na kwenda kulisajili na akakuzuia kulitumia.
Hata kama jina la biashara ni zuri sana na unalipenda,
usipolisajili hauna uhalali wa kulitumia jina hilo.
Uzuri wa Jina la Biashara lina sifa kuu pekee ambayo
ni kutofanana na jina la mtu mwingine.
Na ili kuzuia kutotumiwa na mtu mwingine kwa
kulisajili katika mamlaka husika, hivyo kulipa uhalali jina lako la biashara
nawe utakuwa huru kulitumia wakati wowote ule.
Jina la biashara husajiliwa kwa Msajili wa Biashara
na Makampuni (BRELA). Ada ya Usajili ni sh 20,000/- kiasi ambacho kila
mfanyabishara anao uwezo wa kuipata.
BRELA wamerahisisha sana kwa sasa, ambapo hautakiwi
kufika ofisini kwao, badala yake unaweza kusajili jina lako la biashara na
kukamilisha kwa njia ya mtandao (BRELA ORS).
Kupitia BRELA ORS unaweza kufanya yafuatayo;
a)Usajili wa jina la biashara (Registration of
new business name)
b)Malipo ya ada ya mwaka ya uendeshaji (Payment of
annual maintenance name)
c)Kukoma kwa jina la biashara (Cessation of business
name)
d)Mabadiliko ya taarifa za jina la biashara (Change
of particulars of business name)
e)Uhuishaji wa taarifa mpya za jina la biashara
lililopo (Data update of an existing business name).
Ndani ya kitabu hiki nimekuonyesha mambo mengi
kuhusiana na usajili wa jina la Biashara. Uzuri ni kwamba nimekuonyesha kwa
lugha kwa njia rahisi sana.
Ndani ya kitabu,
utajifunza yafuatayo;
1.
Maana ya Jina la
Biashara
2.
Sifa za jina la
Biashara linalokubalika kisheria na linaloweza kusajilika
3.
Mchango wa jina
la Biashara katika soko la ushindani
4.
Faida 10 za
kusajili jina la biashara
5.
Hatua 10 za
kufuata ili uweze kusajili ili uweze kusajili jina la biashara kwa urahisi
zaidi.
Kitabu hiki kina
thamani ya Tsh 15,000+ Lakini ili kukusaidia leo utakipata kwa Tsh 4,999/=
pekee okoa zaidi ya 10k+ BONYEZA HAPA KUPATA KITABU
Kukipata kitabu
hiki, Tuma Tsh 4,999/= kwenda LIPA NO VODA 5776586 yenye jina la JOSHUA
GOLYAMA. Kisha tutumie uthibitisho whatsApp no +255 764 257 495 na utatumiwa
kitabu ndani ya dakika moja tu.